SOKA-CAF

Mechi za hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa na Shirikisho kuanza Ijumaa

Mabingwa wa taji la Shirikisho barani Afrika mwaka 2016 TP Mazembe
Mabingwa wa taji la Shirikisho barani Afrika mwaka 2016 TP Mazembe STRINGER / AFP

Michuano ya soka hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa na Shirikisho barani Afrika, inachezwa kuanzia siku ya Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Timu 16 zimepangwa katika makundi manne, kila kundi na timu nne.

Mabingwa watetezi wa klabu bingwa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini wataanza kampeni yao dhidi ya Saint George ya Ethiopia siku ya Jumapili.

Mamelodi Sundowns inakumbukwa kuwa klabu ya pili ya Afrika Kusini kushinda taji hilo baada ya kuishinda Zamalek ya Misri kwa mabao 3-1 baada ya mechi mbili za fainali nyumbani na ugenini.

Kocha wa klabu hii Pitso Mosimane amesema wachezaji wake wanakwenda katika mchuano huu wakiwa na uchovu kwa sababu ya mechi za ligi kuu ya soka nchini mwake.

Ratiba Kamili siku ya Ijumaa Mei 12 2017:-

 • ES Tunis (Tunisia) vs Vita Club (DRC)
 • Etoile du Sahel (Tunisia) vs Ferroviario Beira (Msumbiji)
 • USM Alger (Algeria) vs Al Ahli Tripoli (Libya)
 • Al Hilal Omdurman (Sudan) vs Al Merreikh (Sudan)
 • Zamalek (Misri) vs CAPS United (Zimbabwe)
 • Wydad Casablanca (Morocco) vs Cotonsport (Cameroon)

Jumamosi Mei 12 2017:
Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) vs Saint George (Ethiopia)
Al Ahly (Misri) vs Zanaco (Zambia)

Mabingwa watetezi wa taji la Shirikisho mabingwa watetezi TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, itaanza kumenyana dhidi ya Mounana ya Gabon mjini Lubumbashi.

Hata hivyo siku ya Ijumaa, SuperSport United itakabilana na Horoya ya Guinea Conakry.

Mechi nyingine za siku ya Jumapili:-

 • Recreativo do Libolo (Angola) vs Hilal (Sudan)
 • Platinum Stars (Afrika Kusini) vs MC Alger (Algeria)
 • Club Africain (Tunisia) vs Rivers United (Nigeria)

Jumamosi:

 • ZESCO United (Zambia) vs Smouha (Misri)
 • CS Sfaxien (Tunisia) vs Mbabane Swallows (Swaziland)
 • FUS Rabat (Morocco) vs KCCA (Uganda)