AFCON 2017

Tanzania kuanza kampeni ya kutafuta ubingwa wa Afrika dhidi ya Mali

Timu ya taifa ya Guinea kabla ya kuikabili Gabon Mei 14 2017 jijin Port Gentil
Timu ya taifa ya Guinea kabla ya kuikabili Gabon Mei 14 2017 jijin Port Gentil Cafonline

Timu ya taifa ya mchezo wa soka kwa vijana wasiozidi miaka 17 ya Tanzania maarufu kama Serengeti Boys, inaanza kampeni ya kutafuta ubingwa wa Afrika dhidi ya Mali Jumatatu jioni katika uwanja wa Amitie jijini Libreville kuanzia saa kumi na moja na nusu saa za Afrika Mashariki.

Matangazo ya kibiashara

Hii ndio mara ya kwanza kwa Tanzania kushiriki katika michuano hii mikubwa kwa vijana barani Afrika, na mchuano wa leo dhidi ya mabingwa watetezi itapima ubora wake katika michuano hiii.

Serengeti Boys walikuwa na maandalizi ya muda mrefu nchini Morocco na Cameroon, na kucheza mechi kadhaa za kirafiki dhidi ya Cameroon, Ghana na Burundi kabla ya kwenda Gabon.

Tanzania imepangwa katika kundi la B pamoja na Angola na Niger.

Mechi nyingine ya kundi hili kati ya Angola na Niger, itachezwa kuanzia saa mbili usiku.

Mechi za ufunguzi zilichezwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika uwanja wa Port Gentil.

Wenyeji Gabon walianza vibaya baada ya kufungwa na Guinea mabao 5-1 mbele ya rais wao Ali Bongo, huku mabao matatu yakifungwa na Djibril Fandjé Toure.

Hadi kipindi cha mapumziko, Guinea ilikuwa inaongoza kwa mabao 4-0.

Mchuano wa pili wa kundi hilo, Ghana iliishinda Cameroon mabao 4-0 huku Eric Ayiah akifunga mabao 3 katika mchuano huo.

Ratiba inyaofuata kundi la A, Mei 17 2017:-

  • Guinea vs Cameroon
  • Ghana vs Gabon