SOKA-League 1

Jean Michael Seri ndiye mchezaji bora kutoka barani Afrika anayecheza soka nchini Ufaransa

Jean Michaël Seri, mchezaji bora wa soka katika ligi kuu ya soka nchini Ufaransa kutoka barani Afrika
Jean Michaël Seri, mchezaji bora wa soka katika ligi kuu ya soka nchini Ufaransa kutoka barani Afrika Reuters/Eric Gaillard

Mchezaji wa Kimataifa wa timu ya soka ya Ivory Coast Jean Michael Seri anayechezea klabu ya Nice, ametajwa kuwa mchezaji bora kutoka barani Afrika, anayecheza katika ligi kuu ya soka nchini Ufaransa ya Ligue 1.

Matangazo ya kibiashara

Kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 25, aliibuka mshindi mbele ya Ryad Boudebouz kutoka Algeria anayechezea klabu ya Montpellier na Benjamin Moukandjo raia wa Cameroon anayeichezea Lorient.

Seri alianza kuichezea Nice mwezi Juni mwaka 2015 na kucheza mechi zote 38 na kuisaidia klabu yake kumaliza katika nafasi ya nne wakati huo.

Msimu huu, mchezaji huyo ameifungia klabu yake mabao sita na kuisaidia klabu yake kumaliza ya tatu.

Tuzo hii hutolewa kila mwaka na kufadhiliwa  na kituo cha RFI/Fr24 kwa lengo la kumkumbuka mchezaji wa zamani wa  Cameroon Marc- Vivian Foe aliyezirai na kufariki dunia mwaka 2003.

Washindi wa miaka iliyopita
2016: Sofiane Boufal (Morocco/Lille)
2015: Andre Ayew (Ghana/Marseille)
2014: Vincent Enyeama (Nigeria/Lille)
2013: Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon/Saint-Étienne)
2012: Younès Belhanda (Morocco/Montpellier)
2011: Gervinho (Ivory Coast/Lille)
2010: Gervinho (Ivory Coast/Lille)
2009: Marouane Chamakh (Morocco/Bordeaux)