OLIMPIKI 2024

Kamati ya Michezo ya Olimpiki yazuru jijini Paris kuelekea michezo ya 2024

Nembo ya Michezo ya Olimpiki mwaka 2024
Nembo ya Michezo ya Olimpiki mwaka 2024 法新社

Maafisa wa Kamati ya Kimataifa ya michezo ya Olimpiki wanamaliza ziara yao ya siku tatu nchini Ufaransa, kuthathmini uwezo wa jijini la Paris kuwa mwenyeji wa michezo ya mwaka 2024.

Matangazo ya kibiashara

Ziara hii imekuja baada ya kufanya ziara nyingine kama hiyo jijini Los Angeles nchini Marekani na kuthathmini miundo mbinu na utayari wa mji huwa kufanikisha michezo hii.

Kamati hiyo ya wajumbe 11 wakiwa nchini Ufaransa wamezuru maeneo maarufu kama Champs-Elysees na Grand Palais, na eneo la Saint-Denis Kaskazini Mashariki mwa jiji hilo kunakopendekezwa kuwa kijiji cha kuwapa hifadhi maelfu ya wanamichezo.

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya soka Lilian Thuram aliyeisadia nchi yake kunyakua taji la dunia mwaka 1998 ndiye aliyewatembeza maafisa hao kuuona uwanja wa taifa wa Stade de France.

Ushindani ni kati ya jiji la Paris na Los Angeles, na uamuzi wa mwisho kuhusu ni mji upi utashinda, utafahamika tarehe 13 mwezi Septemba jijini Lima nchini Peru.