SOKA-CAF

Tanzania yawabana Mali na kulazimisha sare mechi ya kwanza ubingwa wa Afrika kwa vijana

Tanzania ikimenyana na Mali katika mchuano wa kwanza wa kuwani ubingwa wa Afrika kwa vijana chipukizi chini ya miaka 17
Tanzania ikimenyana na Mali katika mchuano wa kwanza wa kuwani ubingwa wa Afrika kwa vijana chipukizi chini ya miaka 17 Wikipedia

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania chini ya miaka 17 Serengeti Boys, walianza kampeni ya kutafuta ubingwa wa bara Afrika kwa kulazimisha sare ya kutofungana na Mali katika mchuano wa ufunguzi wa kundi B siku ya Jumatatu nchini Gabon.

Matangazo ya kibiashara

Mali walionekana kutawala mchezo huo vipindi vyote viwili lakini wakakosa kutumia vizuri nafasi za wazi walizopata kupachika mabao lakini beki ya Tanzania ilikuwa imara kuzuia nyavu zake kutikitiswa.

Tanzania ilionekana kucheza kwa kujilinda na kucheza kwa umakini kuzuia kufungwa karika mchuano huo wa kwanza, licha ya kutokuwa na mashambulizi mengi kama ilivyokuwa kwa Mali.

Mechi ya ya pili ya kundi hilo, Niger ilionekana kuvunjika moyo baada ya kuongoza kwa mabao mawili, na baadaye kuwapa wapinzani wao fursa ya kusawazisha mabao yote na mchuano huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Matokeo ya michuano ya kundi hili, inamaaisha kuwa kila kitu ina alama moja.

Ratiba ya ijayo Mei 18 2017
Tanzania vs Angola
Niger vs Mali

Michuano hii inaendelea siku ya Jumanne kwa mechi za kundi A.

Guinea walioshinda mechi ya kwanza kwa kuizaba wenyeji Gabon mabao 5-1, inachuana na Cameroon iliyopoteza mechi yake ya kwanza dhidi ya Ghana kwa mabao 4-0.

Gabon nayo itakuwa katika uwanja wa Port Gentil, itakuwa inamenyana na Ghana ambayo inataka kuendeleza rekodi ya ushindi katika michuano hii.

Wenyeji Gabon wanahitaji ushindi kuendelea kushiriki katika michuano hii.