SOKA-AFCON 2017

Fainali ya AFCON kwa vijana: Tanzania kusaka ushindi muhimu dhidi ya Angola

Mataifa yanayoshiriki katika michuano ya Afrika baina ya vijana wasiozidi miaka 17 nchini Gabon
Mataifa yanayoshiriki katika michuano ya Afrika baina ya vijana wasiozidi miaka 17 nchini Gabon Wikipedia

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania ya vijana wasiozidi miaka 17 inarejea tena uwanjani jioni hii katika mechi yake ya pili ya kundi B kutafuta ubingwa wa Afrika katika michuano inayoendelea nchini Gabon.

Matangazo ya kibiashara

Serengeti Boys wanamenyana na Angola katika mchuano muhimu baada ya mechi ya kwanza kulazimisha sare ya 0-0 na mabingwa watetezi Mali.

Mchuano huu unachezwa katika uwanja wa Amitie jijini Libreville kuanzia saa 11 na nusu jioni saa za Afrika Mashariki.

Angola nayo katika mchuano wake wa kwanza, ilitoka nyuma na kulazimisha sare ya mabao 2-2 na Niger.

Kila timu katika kund hili, ina alama 1 na hivyo kuwa na uwezo wa kufuzu.

Siku ya Jumatano, Ghana ilifuzu katika hatua ya nusu fainali baada ya kushinda mechi yake ya pili kwa kuwafunga wenyeji Gabon mabao 5-0.

Mechi ya kwanza, Ghana iliishinda Cameroon kwa mabao 4-0.

Guinea nayo ipo njiani kufuzu baada ya sare ya bao 1-1 na Cameroon katika mechi yake ya pili.