SOKA-CAF

AS Vita Club kutafuta ushindi wa kwanza dhidi ya Mamelodi Sundowns

KCCA ikimenyana na  Club Africain ya Tunisia Mei 23 2017 katika uwanja wa Philip Omondi jijini Kampala
KCCA ikimenyana na Club Africain ya Tunisia Mei 23 2017 katika uwanja wa Philip Omondi jijini Kampala KCCA

AS Vita Club ya DRC inaikaribisha mabingwa watetezi wa taji la klabu bingwa barani Afrika Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika mechi muhimu siku ya Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Mechi hii inachezwa katika uwanja wa Martyrs jijini Kinshasa.

Mamelodi Sundowns inakwenda katika mchuano huu baada ya kutofungana katika mchuano wa kwanza dhidi ya Saint George ya Ethiopia katika mechi za kundi C.

Esperience de Tunis ya Tunisia, inaongoza kundi hili kwa alama 4 baada ya kutofungana Saint George siku ya Jumanne.

Ratiba nyingine za Jumatano:-

CAPS United vs USM Alger
Zanaco vs Wydad Casablanca

Nayo KCCA ya Uganda iliwashangaza Club Africain ya Tunisia kwa mabao 2-1 siku ya Jumanne.

KCCA wakiwa nyumbani katika uwanja wa Philip Omondi jijini Kampala, ilitoka nyuma na kusawazisha bao la kwanza lilikuwa limefungwa na wageni katika dakika 19.

Muda mfupi kabla ya muda wa mapumziko mshambuliaji wa KCCA, Derrick Nsibambi aliisawazishia klabu yake katika  dakika ya 46 ya mchuano huo.

Bao la ushindi lilitiwa kimyani na Tom Masiko katika dakika 63 kipindi cha pili.

Klabu hiyo ya Uganda ni ya pili katika kundi la A kwa alama tatu nyuma na FUS Rabat ya Morroco inayomenyana na Rivers United ya Nigeria siku ya Jumatano.

Mabingwa watetezi TP Mazembe watakuwa ugenini kumenyana na
Horoya ya Guinea.

Mechi ya kwanza, Mazembe wakicheza nyumbani waliishinda CF Mounana ya Gabon kwa mabao 2-0.

Ratiba ya mechi za Jumatano:-

  • Smouha vs Recreativo du Libolo
  • Hilal Obayed vs ZESCO United