Michuano ya French Open kuanza bila ya Serena Williams na Roger Federer
Imechapishwa:
Makala ya 116 ya michuano ya Tennis ya French Open yanaanza kutifua vumbi siku ya Jumapili katika uwanjawa Roland Garros jijini Paris.
Bingwa mtetezi wa michuano ya Australian Open wa upande wa wanawake Serena Williams na bingwa mtetezi wa upande wa wanaume Roger Federer kutoka Switzerland hatawashiriki katika michuano hii.
Serena Williams hatakuwepo kwa sababu ni mjamzito.
Hata hivyo, mabingwa watetezi wa michuao hii kwa upande wa wanaume Novak Djokovic kutoka Serbia na Garbine Muguruza kutoka Uhispania watakuwepo kutetea mataji yao.
Wachezaji wa kiume 32 akiwemo Andy Murray, Novak Djokovich, Stan Wawrinka, Rafael Nadal watapambana katika hatua mbalimbali za mwondoano huku Angelique Kerber, Karolina Pliskova, Simona Halep, Slina Svitolina wakiwa ni miongoni mwa wanawake 32 watakaotoana kijasho katika michuano hii itakayomalizika tarehe 11 mwezi Juni.