TENNIS-MICHEZO

Andy Murray kutafuta ubingwa katika michuano ya French Open

Andy Murray wakati wa mechi aliopoteza dhidi Kevin Anderson katika mzunguko wa8 wa mashindano ya US Open, Septemba 7, 2015 mjini New York
Andy Murray wakati wa mechi aliopoteza dhidi Kevin Anderson katika mzunguko wa8 wa mashindano ya US Open, Septemba 7, 2015 mjini New York AFP/AFP

Bingwa namba moja duniani katika mchezo wa Tennis, Mwingereza Andy Murray, anaanza kampeni ya kutafuta ubingwa French open dhidi ya Stanislas Wawrinka kutoka Uswisi.

Matangazo ya kibiashara

Kwa upande mwengine Bingwa mtetezi Novak Djokovic alipata ushindi wake baada ya kupata kocha mpya Andre Agassi.

Siku ya Jumatatu Mei 29 Rafel Nadal alianza vema baada ya kumshinda Mfaransa Benoit Paire 6-1, 6-4, 6-1 .

"Nina furaha kubwa kurudi uwanjani baada ya kile kilichotokea mwaka uliopita. Ni vizuri kupata faraja", amesema Nadal Bingwa mara 14 wa michuano hii.

Bingwa mtetezi kwa upande wa wanawawake, Mhispania Garbine Muguruza alianza vema baada ya kumshinda Francesca Schiavone kutoka Italia kwa seti za 6,2 6,4 na kufaulu kutinga katika hatua ya pli ya michuano hii.