SOKA

Zambia yaizaba Ujerumani kufuzu robo fainali kombe la dunia kwa vijana

Shabiki wa Zambia katika michuano ya kombe la dunia nchini Korea Kusini
Shabiki wa Zambia katika michuano ya kombe la dunia nchini Korea Kusini cdn.vox

Timu ya taifa ya soka ya Zambia yenye wachezaji chini ya miaka 20, imefuzu katika hatua ya robo fainali kuwania kombe la dunia katika michuano inayoendelea nchini Korea Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Mabingwa hao wa Afrika walitoka nyuma na kuifunga Ujerumani mabao 4-3 katika muda wa nyongeza, baada ya timu zote kutofungana katika muda wa kawaida.

Zambia ilionekana kuwa imeshinda mechi hiyo baada ya kuongoza kwa mabao 3-1 katika dakika ya 89, lakini wachezaji wa Ujerumani Suat Serdar na Jonas Arweiler walifunga mabao ya haraka na kufanya mambo kuwa sare ya mabao 3-3.

Hata hivyo, Shemmy Mayembe alikuwa shujaa wa Zambia, baada ya kufunga bao la nne na la ushindi na kuifanya Chipolopolo kupata ushindi wa mabao 4-3.

Wafungaji wengine wa Zambia ni pamoja na Emmanuel Banda, Enock Mwepu na Fashion Sakala.

Zambia sasa watachuana na Ufaransa au Italia katika hatua ya robo fainali.

Wawakilishi wengine wa Afrika Senegal, watamenyana na Mexico siku ya Alhamisi.

Mbali na Zambia, Uingreza, Uruaguay, Ureno na Venezuela zimefuzu katika hatua ya robo fainali.

Ratiba ya Juni 1 2017:-

  • Mexico vs Senegal
  • Ufaransa vs Italia
  • Marekani vs New Zealand

Robo fainali:-

Juni 04 2017

  • Venezuela vs Mshindi kati ya Marekani na New Zealand
  • Ureno vs Uruguay

Juni 05 2017

  • Mshindi kati ya Ufaransa na Italia vs Zambia
  • Mshindi kati ya Mexico na Senegal vs Senegal.