SOKA-UINGEREZA

Ratiba ya msimu mpya ya ligi kuu nchini Uingereza yatangazwa

Nembo ya ligi kuu nchini Uingereza
Nembo ya ligi kuu nchini Uingereza EPL

Ratiba ya msimu mpya wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza imetangazwa siku ya Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Mabingwa watetezi Chelsea wataanza harakati za kutetea taji lao dhidi ya Burnle siku ya Jumamosi tarehe 12 mwezi Agosti.

Klabu ya Newcastle ambayo imepandishwa daraja nayo itaanza kutafuta ubingwa dhidi ya Tottenham Hotspurs huku Brighton wakianza nyumbani dhidi ya mabingwa wa zamani Manchester City.

Wageni wengine katika ligi hii Huddersfield FC, watasafiri kwenda katika uwanja wa Selhurst Park kumenyana na Crystal Palace.

Ratiba nyingine Agosti 12 2017:

  • Arsenal v Leicester City
  • Everton v Stoke City
  • Manchester United v West Ham United
  • Southampton v Swansea City
  • Watford v Liverpool
  • West Bromwich Albion v Bournemouth