SOKA-KOMBE LA DUNIA URUSI 2018

Ripoti:Urusi inapiga hatua katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi viwanjani

Nembo ya kombe la dunia nchini Urusi 2018
Nembo ya kombe la dunia nchini Urusi 2018 FIFA.COM

Urusi inapiga hatua katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi katika mchezo wa soka kuelekea michuano ya kombe la dunia mwaka 2018.

Matangazo ya kibiashara

Mafanikio haya yamebainishwa na taasisi ya bara Ulaya FARE inayopiga vita ubaguzi wa rangi katika mchezo wa soka.

Taasisi kama hii nchini Urusi SOVA pia imethibitisha hili baada ya kutoa ripoti yake.

Msimu wa ligi kuu ya soka nchini humo msimu huu, kumekuwa na visa 89 ikilinganishwa na misimu miwili iliyopita wakati kulikuwa na idadi kubwa ya ubaguzi wa rangi hasa kwa wachezaji weusi.

Hivi karibuni, mchezaji kutoka barani Afrika alilalamika kudhalalishwa kwa misingi ya rangi alipokuwa anashiriki katika ligi kuu nchini humo.

Ripoti hii imekuja wakati huu, nchi hiyo inapojiandaa kuwa mwenyeji wa michuano ya kutafuta ubingwa wa mabara kuanzia siku ya Jumamosi.

Shirikisho la soka duniani FIFA, limeitaka Urusi kuhakikisha kuwa visa vya ubaguzi wa rangi havishuhudiwi nchini humo kipindi cha kombe la dunia.