SOKA-CAF-KLABU BINGWA-SHIRIKISHO

Al Ahly kutafuta nafasi ya kufuzu hatua ya mwondoano

Klabu ya Al Ahly ya Misr katika mojawpao ya mechi yake iliyopita.
Klabu ya Al Ahly ya Misr katika mojawpao ya mechi yake iliyopita. Wikipedia

Klabu ya soka ya Al Ahly nchini Misri ina nafasi ya kufuzu katika hatua ya mwondoano kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika ikiwa itaishinda Wydad Casablanca nchini Morocco siku ya Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Itakuwa mara ya kwanza kufika katika hatua hiyo baada ya kufanya hivyo mwaka 2013 na kunyakua taji hilo.

Kocha wa Alhly Hossam El Badry ambaye pia ni mchezaji wa zamani amesema mashabiki wa klabu hiyo wanataka ushindi kwa sababu wanaona wamelikosa taji hilo kwa muda mrefu.

Ahly na Zanaco kutoka Zambia zinaongoza kundi la D kwa alama saba baada ya mechi tatu.

Wydad Casablanca ni wa tatu kwa alama tatu huku Coton Sport ya Cameroon ikiwa haina alama katika kundi hilo.

Ratiba:-

Taji la Shirikisho na klabu bingwa:

Klabu bingwa

Jumanne: Al Merrikh v Ferroviario Beira

Jumatano : Al Ahly Tripoli v CAPS Utd

Jumatano: Al Hilal v Etoile du Sahel

Jumatano: USM Alger v Zamalek

Jumanne: AS Vita Club v Saint George

 

Jumatano : Coton Sport v Zanaco

Jumatano: Esperance v Mamelodi Sundowns

Jumatano: Wydad Casablanca v Al Ahly