SOKA-FUFA-UGANDA

Kasule kuomba msaada wa FIFA baada ya kuzuiwa kuwania urais wa FUFA

Mujib Kasule aliyekuwa anataka kuwania urais wa Shirikisho la soka nchini Uganda FUFA
Mujib Kasule aliyekuwa anataka kuwania urais wa Shirikisho la soka nchini Uganda FUFA Wikipedia

Mpinzani pekee wa rais wa sasa wa Shirikisho la soka nchini Uganda amekosa idhini ya kuwania urais wa FUFA tarehe 5 mwezi Agosti.

Matangazo ya kibiashara

Kamati maalum inayosimamia Uchaguzi huo imesema Mujib Kasule alishindwa kutimiza vigezo muhimu vinavyotakiwa ili kuwa mgombea.

Hii inamaana kuwa rais wa sasa Moses Magogo hatakuwa na mpinzani wakati wa Uchaguzi huo ikiwa mambo yatasalia kuwa hivi.

Hata hivyo, Kasule akizungumza na wanahabari siku ya Jumanne jijini Kampala, amesema atakata rufaa katika Shirikisho la soka duniani FIFA kulalamikia kuondolewa kwake.

Aidha, amesema kuwa ikiwa FIFA haitafanya maamuzi ya kumruhusu kuwania wadhifa huo, atakwenda Mahakamani kutaka kurejeshwa katika kinyanganyiro hicho.

Kasule amemshutumu Magogo kwa kuendelea kuharibu soka nchini humo lakini pia kumzuia kupitishwa na Kamati hiyo ya Uchaguzi.

Magogo amekanusha madai hayo.