FIFA-SOKA-MABARA

Matumaini ya Cameroon kusonga mbele michuano ya mabara yadidimia

Mchezaji wa Cameroon akimenyana na wenzake wa Australia katika mchuano muhimu wa kutafuta ubingwa wa mabara
Mchezaji wa Cameroon akimenyana na wenzake wa Australia katika mchuano muhimu wa kutafuta ubingwa wa mabara cdn-s3.si.com

Matumaini ya timu ya taifa ya Cameroon kufuzu katika hatua ya robo fainali kuwania kombe la dunia la mabara imedidimia, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Australia katika mchuano wake wa pili Alhamisi usiku.

Matangazo ya kibiashara

Simba wa Nyika, walianza vema mchuano huo kwa kupata bao la ufunguzi katika kipindi cha kwanza kupitia mshambuliaji wake Andre-Frank Zambo Anguissa.

Hata hivyo, nahodha wa Australia Mark Milligan aliisawazishia nchi yake katika dakika ya 60 ya mchuano huo.

Sare hii inaifanya Cameroon kuwa kibarua kigumu sana kufuzu katika hatua hii, inahitaji kuishinda Ujerumani na kuomba kuwa Chile inaishinda Australia.

Kundi la B, Chile wanaongoza kwa alama 4 sawa na Ujerumani huku Australia na Cameroon.

Mechi za kutamatisha hatua ya makundi zitachezwa mwishoni mwa juma hili.

Jumamosi Juni 24 2017

  • Mexico vs Urusi
  • New Zealand vs Ureno

Jumapili Juni 25 2017

  • Ujerumani vs Cameroon
  • Chile vs Australia.