DRC-FECOFA

Wanawake nchini DRC kumenyana kutafuta ubingwa wa Taifa

Mipira
Mipira FECOFA

Shirikisho la soka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FECOFA), limetangaza droo ya kutafuta ubingwa wa klabu bora kwa upande wa wanawake nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Michuano hiyo itaanza kuchezwa siku ya Jumapili tarehe 25 mwezi huu wa Juni na kumalizika tarehe 8 jijini Kinshasa.

Rais wa soka la wanawake nchini humo Lyly Tshimpimpu, ametangaza kuwa mchuano wa kwanza utakuwa kati ya mabingwa watetezi Mbuji-Mayi FC dhidi ya DCMP Bikira de Lubumbashi.

Timu hizi mbili zilikutana mwaka uliopita katika fainali ya kutafuta bingwa wa makala ya tisa ya michuano hii inayolenga kuinua soka la wananwake nchini humo.

Hata hivyo, waandalizi wa michuano hii ya 10 wanaonya kuwa kwa sababu ya uhaba wa fedha huenda timu nyingine kutoka mikoani zikashindwa kufika jijini Kinshasa kushiriki katika michuano hiyo.

Ratiba ya michuano nyingine:-

FCF Avenir (Kinshasa) vs Bafana Bafana (Lubumbashi)

JS Kolwezi (Kolwezi) vs Promo Sport (Kongo Central)

BOA (Maniema) vs Etoile (Kivu Kusini )

31st CPC (Mbuji-Mayi) vs Star of Morning (Kinshasa)

FCF Okapi (Tshopo) vs FCT Gora (Kongo Central)

As Victoire (Kananga) vs FCF Bilenge (Kinshasa)