SOKA-AFCON-MICHEZO

Uchunguzi wa RFI: Ni michuano ya Kombe lipi la Mataifa ya Afrika unayohitaji?

RFI / Pierre René-Worms

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) litajadili hatma ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), kuanzia Julai 18 hadi Julai 21, 2017 nchini Morocco. Michuano ya AFCON inayopigwa kila baada ya miaka miwili, inaweza kuchezwa kila baada ya miaka minne? Michuano hii inaweza kupigwa mnamo mwezi Juni na Julai badala ya mwezi Januari na Februari? Jibu ukituma ujumbe wako kwa uchunguzi RFI kuanzia Juni 22 hadi Julai 17 ambapo matokeo yatatangazwa Julai 18.