CAMEROON-UJERUMANI-SOKA

Cameroon yaaga mashindano ya Kombe la Shirikisho

Timu ya taifa ya Cameroon imebanduliwa na Ujerumani kwenye michunao ya Kombe la Shirikisho, baada ya kufungwa 3-1.
Timu ya taifa ya Cameroon imebanduliwa na Ujerumani kwenye michunao ya Kombe la Shirikisho, baada ya kufungwa 3-1. REUTERS/Kai Pfaffenbach

Timu ya taifa ya Cameroon, Simba wa Nyika, wamekubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Ujerumani na hivyo kujikuta wameaga mashindano ya Kombe la Shirikisho. Vincent Aboubakar aliifungia timu yake ya Cameroon bao moja la kufuta machozi. Mabingwa wa Afrika walikua hawana bahati ya kuendelea katika michuano hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Simba wa Nyika walikua hawana jipya kwa kugeuza karata katika mchezo huo. Baada ya kupoteza dhidi Chile (2-1) katika mechi yake ya kwanza na kukubali kutoka sare ya 1-1 dhidi Australia, Cameroon imekubali kichapo cha mabao 3-1 kwa mechi yake ya mwisho. Mabingwa wa Afrika walikua na pointi moja tu katika mechi tatu na hivyo kumaliza mwisho katika kundi lao.

Pamoja na kuanza na bidii kwa mechi hii dhidi ya mabingwa wa dunia licha ya mchezaji Christian Bassogog kuonyesha ujuzi wake, Cameroon hawakuweza kujitetea hata kipindi kimoja cha mchezo. Kwa sababu tangu kuanza kwa kipindi cha pili, Mannschaft, timu ya taifa ya Ujerumani, ilianza kwa kasi na kufungua bao la kwanza kupitia mchezaji wakeKareem Demirbay katika dakika ya 48 baada ya kupata pasi nzuri. Hata hivyo Cameroon walijikuta wakicheza 10 baada ya kufukuzwa kwa mchezaji Ernest Mabouka. Bao la pili lilifungwa muda mfupi baadae katika dakika 66 na mchezaji Timo Werner. Ingawa Vincent Abubakar alifunga bao la kufuta machozi katika dakika ya 78, Ujerumani iliongeza bao la tatu kupitia mchezaji Werner katika dakika 81.

Kushindwa huku kwa timu ya taifa ya Cameroon kumedhihirisha ubovu wa timu hii ambayo ilipata kwa usubufu ushindi wa kushangaza katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Januari.

Katika michuano hii ya Kombe la Confederations,vujana wa Hugo Broos hawanekana kuwa na kiwango cha kukabiliana na wapinzani wao, hata kama walitoka sare ya kufungana 1-1 na Australia. Lakini kama safu ya ulinzi ilikaribishwa katika michuano ya AFCON iliopita, wakati huu safu hii ilishindwa kudhibiti mashambulizi ya wapinzani. Camroon iliingizwa mabao 6 katika mechi tatu). Zaidi ya yote, ni kukera kwamba Cameroon kuwa fiska katika mashindano yao. timu hii ilionekana dhaifu upande wa washambuliaji. Katika mechi tatu, mshambuliaji mmoja tu Aboubakar alipata nafasi nzuri ya kuweka mpira wavuni. Bao la pili la mashindano ya Simba wa Nyika lilipatikan akwa kazi nzuri ya kiungo wa kati mlinzi, Zambo Anguissa.

Mchunao wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho lutazikutanisha Ujerumani na Mexico (siku ya Alhamisi saa 20:00 usiku) na Ureno na Chile (Jumatano, saa 20:00 usiku).