FIFA-KOMBE LA MABARA

Mataifa yatakayocheza nusu fainali ya mabara yafahamika

Wachezaji wa Chile wakisherehekea bao dhidi ya Australia Juni 25 2017
Wachezaji wa Chile wakisherehekea bao dhidi ya Australia Juni 25 2017 FIFA.COM

Ureno na Chile zitamenyana katika hatua ya nusu fainali kuwania ubingwa wa kombe la dunia la mabara katika mchezo wa soka, mechi itakayochezwa siku ya Jumatano katika uwanja wa Azan nchini Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Chile ilifuzu katika hatua hiyo baada ya kumaliza katika nafasi ya pili katika kundi  B kwa alama 5 baada ya kumaliza mchuano wake wa mwisho dhidi ya Australia kwa sare ya bao 1-1.

Ureno nao walifuzu baada ya kuongoza kundi la A kwa alama 7.

Nusu fainali ya pili itachezwa siku ya Alhamisi, kati ya Ujerumani na Mexico.

Mexico ilimaliza katika nafasi ya pili katika kundi B lakini Ujerumani walimaliza vema mechi zao za hatua ya makundi dhidi ya wawakilishi wa Afrika Cameroon kwa kuwashinda mabao 3-1 hapo jana.

Fainali iatchezwa siku ya Jumapili mjini Saint Petersburg huku mshindi akitarajiwa kupata kombe la Dola za Marekani Milioni 5.