SOKA-COSAFA

Tanzania yaanza vema kampeni ya kutafuta taji la COSAFA

Mchezaji wa Tanzania akimenyana na mwenzake wa Malawi katika mchuano wa kwanza wa COSAFA Juni 25 2017 nchini Afrika Kusini
Mchezaji wa Tanzania akimenyana na mwenzake wa Malawi katika mchuano wa kwanza wa COSAFA Juni 25 2017 nchini Afrika Kusini COSAFAMEDIA

Tanzania ilianza vema michuano ya soka kuwania ubingwa wa  COSAFA baina ya mataufa ya Kusini mwa bara Afrika iliyoanza jana nchini Afrika Kusini kwa kuishinda Malawi mabao 2 kwa 0.

Matangazo ya kibiashara

Huu ndio ushindi wa kwanza kwa Tanzania ambao wamealikwa katika mashindano haya, baada ya kujaribu kufanya hivyo mwaka 1997 na 2015.

Mabao yote ya Tanzania yalitiwa kimyani na mchezaji Yahya Ramadhani.

Angola nao walianza vema kwa kuishinda Mauritius  bao 1-0 lililofungwa na Augusto Quibeto katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo.

Tanzania inaongoza kundi la A kwa alama 3 mbele ya Angola ambayo pia ina alama tatu lakini tofauti ya bao moja.

Taifa Stars itamenyana na Angola kesho katika mchuano wake wa pili katika kundi hili huku Malawi wakimenyana na Mauritius.

Mshindi wa kundi hili atamenyana na Afrika Kusini katika hatua ya robo fainali.

Ratiba ya kundi B:

  • Msumbiji vs Zimbabwe
  • Madagascar vs Ushelisheli

Mshindi wa kundi hili atapambana na Swaziland katika hatua ya robo fainali tarehe mbili mwezi Julai.