FIFA-SOKA-MABARA

Chile yailaza Ureno kufuzu fainali kutafuta ubingwa wa Mabara

Kipa wa timu ya taifa ya Chile Claudio Bravo akionesha akizuia mpira kuingia wavuni Juni 28 2017
Kipa wa timu ya taifa ya Chile Claudio Bravo akionesha akizuia mpira kuingia wavuni Juni 28 2017 FIFA.COM

Timu ya taifa ya soka ya Chile imefuzu katika hatua ya fainali kuwania taji la dunia la mabara.

Matangazo ya kibiashara

Wawakilishi hao kutoka Amerika Kusini, walifuzu baada ya kuwafunga Ureno mabao 3-0 kupitia mikwaju ya penalti Jumatano usiku.

Mchuano huo wa nusu fainali ulikwenda katika hatua ya penalti baada ya kumaliza kwa muda wa kawaida na ule wa nyongeza kwa kutofungana.

Kipa wa Chile anayeichezea klabu ya Manchester United Claudio Bravo, alionesha umaahiri wake kwa kuzuia penalti za wachezaji wa Ureno, Ricardo Quaresma, Joao Moutinho na Nani.

Chile nayo ilipata ushindi wake kupitia wachezaji wake Arturo Vidal, Charles Aránguiz na Alexis Sánchez.

Baada ya ushindi huo, Chile sasa inasubiri mshindi kati ya Ujerumani na Mexico watakaomenyana katika nusu fainali ya pili usiku wa leo.

Fainali ya mchezo huu itachezwa siku ya Jumapili katika uwanja wa Krestrovsky mjini Saint Petersburg nchini Urusi.

Mshindi atatuzwa kombe pamoja na Dola za Marekani Milioni tano.