SOKA
Wachezaji wa klabu ya Asante Kotoko wakumbwa na ajali ya barabarani
Imechapishwa:
Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine kujeruhiwa baada ya gari la klabu ya Asante Kotoko nchini Ghanam kuhusika katika ajali ya barabarani.
Matangazo ya kibiashara
Shirikisho la soka nchini Ghana limesema wachezaji hao walikuwa wanasafiri kurudi mjini Kumasi baada ya mechi muhimu ya ligi kuu jijini Accra dhidi ya Inter Allies.
Asante Kotoko inashikilia nafasi ya nne katika msururu wa ligi kuu nchini humo.
Basi la klabu hiyo lilikuwa limewabeba abiria 35, ambao walikuwa ni wachezaji na maafisa wa klabu hiyo.
Ripoti zinasema basi hilo liligongana na lori lililokuwa limebeba mchele.