Mashindano ya riadha ya dunia kwa vijana yamalizika nchini Kenya

Sauti 23:31
Wanariadha wa Kenya walivyoshinda mbio za Mita 800  kuruka viunzi na maji
Wanariadha wa Kenya walivyoshinda mbio za Mita 800 kuruka viunzi na maji www.iaaf.org

Kenya imefanikiwa kuandaa mashindano ya dunia ya riadha kwa vijana wasiozidi miaka 18.Mashindano haya yamekuwa yakifanyika kwa muda wa siku tano zilizopita katika uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani jijini Nairobi. Afrika Kusini ilimaliza ya kwanza kwa medali 11, ikifutawa na China pia kwa medali 11. Cuba ilimaliza ya tatu huku Kenya ikimaliza ya nne kwa medali nyingi ambazo ni 15 lakini ikapata medali 4 ya dhahabu.Tunachambua mashindano haya.