LIGI KUU DRC

Kati ya TP Mazembe na AS VIta Club, nani ataibuka bingwa ?

Wachezaji wa klabu ya AS Vita Club nchini DRC
Wachezaji wa klabu ya AS Vita Club nchini DRC twitter.com/asvitaofficiel

TP Mazembe wanamenyana na AS Vita Club katika mchuano wa mzunguko wa mwisho katika uwanja wa Kamalondo mjini Lubumbashi kuwania ubingwa wa taji la ligi kuu ya soka nchini humo msimu huu.

Matangazo ya kibiashara

Kuelekea katika mchuano huu, timu zote mbili zinatoshana nguvu kwa alama 30, baada ya mechi 13 kuelekea mzunguko wa mwisho ili kumaliza mzunguko wa 14.

Mbali na timu hizi mbili, timu zingine sita ambazo ni DC Motema Pembe, Don Bosco, Sanga Balende, Muungano, Bukavu Dawa na FC Ranaissance, zimekuwa zikichuana kushinda ligi kuu nchini humo msimu huu.

Kuelekea mchuano huo wa mwisho kati ya Mazembe na AS Vita Club, timu zote mbili zimeshinda mechi tisa, kwenda sare mara tatu na kupoteza mchuano mmoja.

Mshindi siku ya Jumatano ataiwakilisha nchI hiyo katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika msimu ujao, huku mshindi wa pili akicheza katika michuano ya Shirikisho.

DC Motema Pembe ambayo ilikuwa mbioni kutafuta ubingwa msimu huu, itamaliza katika nafasi ya tatu kwa alama 27 baada ya kushinda mechi nane, kwenda sare mechi  tatu na kufungwa michuano mingine mitatu.