SOKA-ULAYA

Everton na AC Milan wasonga mbele klabu Bingwa Ulaya

Mara ya mwisho AC Milan kutoa kufunga mabao mengi nyumbaniilikuwa ushindi wake wa bao 8 dhidi ya Union Luxembourg mwaka 1962-1963.
Mara ya mwisho AC Milan kutoa kufunga mabao mengi nyumbaniilikuwa ushindi wake wa bao 8 dhidi ya Union Luxembourg mwaka 1962-1963. RFI/Pierre René-Worms

AC Milan wamewapiga bao 6 Shkendija kutoka Macedonia, huku Everton wakijiweka katika nafasi nzuri hatua ya makundi kufuzu klabu bingwa Ulaya, baada ya kuwashinda Hajduk Split bao 2-0.

Matangazo ya kibiashara

Andre Silva ambaye AC Milan aliyenunuliwa kutoka Porto amefunga mabao mawili peke yake.

Fabio Borini kutoka Sunderland pia amefunga goli lake la kwanza, Luca Antonelli na Riccardo Montolivo nao pia waliziona nyavu za Shkendija.

Mechi kati ya Everton na Hajduk Split ilisimama kwa dakika kadhaa kutokana na vurugu za mashabiki.

Katika dakika ya 33 ya mchezo, mashabiki wa Hajduk walisogea uwanjani na kurusha vitu.

Dakika tatu kabla ya vurugu kutokea Michael Keane alikuwa amewachapa bao la kwanza, na mara baada ya kutuliza vurugu zao Idrissa Gueye akawachapa la pili dakika ya 45.

Meneja wa Everton Ronald Koeman amesema amesikitishwa na tukio hilo ingawa hakujua ni nini kimetokea.

Katika mchezo mwengine, klabu ya Ajax wawalifungwa bao 1-0 na Rosenborg kutoka Norway.