MANCHESTER UNITED

Zlatan Ibrahimovic arejea Manchester United

Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic
Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic Reuters/Andrew Yates

Mshambuliaji wa Kimataifa kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovic , ameungana tena na klabu ya Uingereza ya Manchester United.

Matangazo ya kibiashara

Ibrahimovic ambaye amekuwa akicheza soka nchini Ufaransa katika klabu ya Paris Saint Germain, ametia saini mkataba wa mwaka mmoja.

Mchezaji huyo ambaye  amekuwa akisumbuliwa na jeraha hivi karibuni, amesema amerejea Old Trafford kumaliza aliyoanzisha.

Aidha, ameongeza kuwa  hata kabla ya kuondoka kwake, uongozi wa klabu ya Manchester United haukutaka aondoke.

Mchezaji huyu wa zamani wa Barcelona wakati alipoichezea Manchester United klabu ya kuondoka, aliifungia mabao 28 baada ya mechi 46 na kuisaidia kunyakua taji la Euro League na ligi kuu nchini Uingereza.

Kocha Jose Mourinho amesema amefurahi kumwona tena Ibrahimovic katika klabu hiyo na sasa anaungana na Romelu Lukaku ambaye pia alisajiliwa msimu huu katika klabu hiyo.