ARSENAL

Arsenal yakataa kuruhusu kuondoka kwa Alexis Sanchez

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Alexis Sanchez.
Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Alexis Sanchez. Arsenal.com

Klabu ya Arsenal nchini Uingereza imekataa Pauni Milioni 50 kutoka kwa Manchester City ili kumuuza mshambuliaji wake Alexis Sanchez.

Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Chile aliongezewa mkataba wa kuendelea kuichezea klabu hiyo mwaka huu baada ya kuiwakilisha nchini yake katika michuano ya dunia ya Shirikisho nchini Urusi.

Sanchez mwenye umri wa miaka 28, aliifungia Arsenal mabao 24 na amekuwa akisema angependa kwenda kuichezea klabu ya Manchester City inayofunzwa na Pep Guardiola.

Sanchez aliwakasirisha mashabiki wa Arsenal baada ya kuonekana akitabasamu wakati klabu yake ikifungwa.

Kocha Arsene Wenger amekuwa katika kipindi kigumu baada ya kufungwa na Liverpool mabao 4-0 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ripoti zinasema kuwa kocha wa Arsenal, alitaka Manchester City ikubali kumwachia Sergio Aguero aje kuichezea klabu hiyo, wakati huu dirisha dogo la usajili lilifungwa Alhamisi usiku.

Mbali na Sanchez, mchezaji mwingine wa Arsenal ambaye anaonekana Alex Oxlade-Chamberlain akionekana pia kutaka kuondoka katika klabu hiyo.

Wakati uo huo, klabu ya Everton imekataa kitita cha Pauni Milioni 25 kumnunua mchezaji wake Ross Barkley.

Hata hivyo, Barkley anaweza kuhama ikiwa kutakuwa na mwafaka katika mazungumzo kati ya pande hizo mbili.