TENNIS-US OPEN

Venus Williams afuzu nusu fainali ya US Open

Mchezaji Venus Williams akishangilia baada ya kutinga hatua ya nusu fainali ya US Open kwa kumfunga Petra Kvitova. Sep 5, 2017
Mchezaji Venus Williams akishangilia baada ya kutinga hatua ya nusu fainali ya US Open kwa kumfunga Petra Kvitova. Sep 5, 2017 Jerry Lai-USA TODAY Sports

Bingwa mara saba wa mashindano ya Kimataifa ya Tennis Venus Williams kutoka Marekani, amefuzu katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la US Open.

Matangazo ya kibiashara

Venus mwenye umri wa miaka 37, alifika katika hatua hiyo baada ya kumshinda bingwa mara mbili wa mashindano ya Wimledon nchini Uingereza, Petra Kvitova kwa seti za 6-3, 3-6, 7-6 (7/2).

Mchuano wa nusu fainali utawakutanisha kati ya Venus Williams na Sloane Stephens kuelekea katika hatua ya fainali siku ya Jumamosi.

Venus amesema amefurahi sana kufuzu katika hatua hiyo na mchuano wa nusu fainali, atacheza kwa furaha na utulivu huku Kvitova akionekana kukata tamaa kuwahi kushinda taji la US Open.

Kwa upande wa wanaume, Kevin Anderson kutoka Afrika Kusini, alifika katika hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza na sasa atamenyana na Mhispania Pablo Carreno Busta.

Siku ya Jumatano, Roger Federer kutoka Uhispania atamenyana na Andrey Rublen kutoka Urusi, huku Roger Federer kutoka Uswizi akijiandaa kupambana na Juan Martin del Porto wa Argentina.