OLIMPIKI 2024-2028

Jiji la Paris sasa rasmi kuwa mwenyeji michezo ya Olimpiki 2024

Mnara maarufu wa Paris ukiwa umepambwa na nembo za Olimpiki kuashiria kuwa mwenyeji wa michezo ya mwaka 2024
Mnara maarufu wa Paris ukiwa umepambwa na nembo za Olimpiki kuashiria kuwa mwenyeji wa michezo ya mwaka 2024 GONZALO FUENTES / Reuters

Baada ya kusubiri kwa muda kudogo hatimaye jiji la Paris nchini Ufaransa limethibitishwa kuwa muandaaji wa michezo ya Olimpiki kwa mwaka 2024.

Matangazo ya kibiashara

Mbali na jiji la Paris kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki ya mwaka 2024 jiji la Los Angeles nchini Marekani nalo litakuwa mwenyeji wa michezo ya mwaka 2028.

Tangazo hili limekuwa ni habari nzuri kwa kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC ambayo imeendelea na jitihada za kujisafisha kutokana na kashfa za rushwa ambazo zinaikabili kamati hiyo hasa katika utoaji wa zabuni ya kuandaa michezo hiyo.

Katika zoezi ambalo lilitawalia na tambo za kila aina, wajumbe wa kamati ya Olimpiki kwa kauli moja walipiga kura ya ndio kuidhinisha jiji la Paris na Los Angeles kuwa wenyeji wa michezo ya mwaka 2024 na 2028.

A prefeita de Paris, Anne Hidalgo, Thomas Bach, presidente do Comitê Olímpico Internacional (COI), no centro, e à direita o prefeito de Los Angeles, Eric Garcetti, em 13 de setembro de 2017.
A prefeita de Paris, Anne Hidalgo, Thomas Bach, presidente do Comitê Olímpico Internacional (COI), no centro, e à direita o prefeito de Los Angeles, Eric Garcetti, em 13 de setembro de 2017. REUTERS/Mariana Bazo

Kuliibuka shamrashamra za aina yake kutoka kwa wajumbe wa pande zote mbili ambao kimsingi toka mwezi Juni mwaka huu walikubaliana kupeana kijiti kwa nyakati tofauti na kukubaliana nani atakaeanza kuwa mwenyeji wa michezo ya mwaka 2024.

Rais wa kamati ya Olimpiki Thomas Bach ambaye alikuwa kwenye shinikizo kutangaza washindi wa zabuni za mwaka 2024 na 2028 kwa pamoja, amepongeza namna mchakato wa kuwapata wazabuni hao ulivyofanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Meya wa jiji la Los Angeles Eric Garcetti amesema “hili lilikuwa jibu sahihi, ilikuwa inahusu usawa na urafiki na kupata mshindi atakeridhia na kuridhiwa”.

Hatua hii imekuwa rahisi kufikiwa toka kamati ya Olimpiki IOC izishawishi nchi za Ufaransa na Marekani kuruhusu miji hito kuandaa michezo ya Olimpiki kwa kufuatana hatua ambayo majiji ya Paris na Los Angeles yalikubali.