UHISPANIA-BARCELONA-SOKA

Oscar Grau: Barcelona itaendelea kushiriki katika La Liga

Wachezaji wa FC Barcelona wakishangilia baada ya mchezo wao na PSG ambapo wameweka historia kwenye michuano hiyo. Machi 8, 2017.
Wachezaji wa FC Barcelona wakishangilia baada ya mchezo wao na PSG ambapo wameweka historia kwenye michuano hiyo. Machi 8, 2017. Reuters / Albert Gea Livepic

Mkurugenzi Mkuu wa klabu ya soka ya Barcelona Oscar Grau licha ya kuwepo kwa mzozo wa kisiasa nchini Uhispania na jimbo la Catalonia kujitenga, klabu ya Barcelona, itaendelea kushiriki katika ligi kuu ya La Liga.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu huyo amesema hata iwapo itakuwa rasmi kuwa jimbo la Catalonia ambalo mji wake ni Barcelona na makao makuu ya klabu hiyo, klabu hiyo itaendelea kucheza soka nchini Uhispania.

Hayo yanajiri wakati Rais wa Catalonia Carles Puigdemont, siku ya Jumanne alisaini hati ya kujitenga kwa jimbo la Catalonia, akisita kutangaza uhuru wa eneo hilo.

Serikali kuu ya Uhispania imetishia kufuta kujitawala kwa jimbo hilo iwapo itahitajika kwa maslahi ya taifa nzim ala Uhispania.