UFARANSA-UJERUMANI-SOKA

Ufaransa kupepetana na Ujerumani Novemba 14

Timu ya taifa ya Ufaransa " Les Bleus" katika uwanja wa soka wa Stade de France kabla ya mechi.
Timu ya taifa ya Ufaransa " Les Bleus" katika uwanja wa soka wa Stade de France kabla ya mechi. ©REUTERS/Darren Staples Livepic

Timu ya taifa ya soka ya Ufaransa na Ujerumani, zitamenyana mjini Cologne katika mchuano wa Kimataifa wa kirafiki tarehe 14 mwezi Novemba.

Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la soka nchini Ufaransa limetangaza tarehe hii, na mchuano huo utakuwa ni kama nusu fainali ya kuwania taji la bara Ulaya mwaka 2016, mchuano ambao Ufaransa walishinda kwa mabao 2-0, mabao yote mawili yakifungwa na Antoine Griezmann.

Mchuano huu umetangazwa pia baada yas Ufaransa kufuzu katika fainali ya kombe la dunia mwaka ujao, hapo jana baada ya kusihinda Belarus mabao 2-1.

Ujerumani pia imefuzu katika fainali hiyo. Mchuano huu utatumiwa kama maandalizi muhimu kabla ya kwenda nchini Urusi.