Pata taarifa kuu
KENYA-GOR MAHIA-SOKA

Gor Mahia kukabidhiwa ubingwa wa ligi kuu Kenya

Klabu ya Kenya ya Gor Mahia.
Klabu ya Kenya ya Gor Mahia. Twitter. com/ Gor Mahia
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Klabu ya Gor Mahia itakabidhiwa rasmi ubingwa wa ligi kuu nchini Kenya tarehe 18 mwezi Novemba mjini Kisumu. taarifa hii imethibitishwa na rais wa klabu hiyo Ambrose Rachier.

Matangazo ya kibiashara

Gor Mahia ilishinda ubingwa wa ligi kuu nchini Kenya kwa mara ya 16, mechi nne kabla ya kumalizika kwa msimu wa ligi kuu.

K’Ogalo itamenyana na Sony Sugar katika mchuano wake wa mwisho, siku ambayo watakabidhiwa kombe hilo.

Uongozi wa Gor Mahia ulikosa kupata nafasi ya klabu hiyo kucheza mechi hiyo katika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani na hivyo kulazimika kwenda mjini Kisumu, Magharibi mwa nchi hiyo.

Gor Mahia itawakilisha nchi hiyo kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika mwaka ujao.

Mwaka 1987, Gor Mahia ilinyakua taji la Afrika, matokeo ambayo hayajaonekana katika siku za hivi karibuni.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.