KENYA-ZAMBIA-MICHEZO-SOKA

Harambee Stars kumenyana na Chipolopolo katika mechi ya kirafiki

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars.
Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars. youtube

Timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars, itamenyana na Chipolopolo ya Zambia katika mchuano wa Kimataifa wa kirafiki tarehe 14 mwezi Novemba jijini Nairobi.

Matangazo ya kibiashara

Mchuano huo uliokuwa umepangwa kupigwa dhidi ya Rwanda tarehe 11 lakini, umesitishwa kwa sababu Rwanda inajiandaa kucheza na Ethiopia katika mchuano wa kufuzu fainali ya CHAN baada ya kujiondoa kwa Misri.

Mara ya mwisho kwa Zambia kucheza na Kenya ilikuwa ni mwaka 2016 wakati wa michuano ya kufuzu kucheza fainali ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika.

Mechi ya kwanza, katika uwanja wa Nyayo, Zambia ilishinda mabao 2-1 huku ikipata sare ya bao 1-1 mjini Ndola.

Michuano ya hivi karibuni, Kenya ilipoteza dhidi ya Thailand na Iraq.