SOKA-CECAFA-KENYA

Michuano ya CECAFA kuanza Jumapili nchini Kenya

Kikosi cha timu ya taifa ya Eritrea katika mashindano yaliyopita nchini Kenya
Kikosi cha timu ya taifa ya Eritrea katika mashindano yaliyopita nchini Kenya AFP

Michuano ya soka kuwania taji la Afrika Mashariki na Kati CECAFA, inatarajiwa kuanza siku ya Jumapili nchini Kenya.

Matangazo ya kibiashara

Mataifa 10 yatashiriki katika michuano hii na tayari droo ya hatua ya makundi imeshatangaza.

Kundi A: Kenya, Rwanda, Libya, Tanzania na Zanzibar

Kundi B: Uganda, Zimbabwe, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.

Mechi ya ufunguzi itakuwa kati ya wenyeji Kenya na Rwanda lakini mechi nyingine siku hiyo ya kwanza itakuwa ni kati ya Libya na Tanzania.

Michuano hiyo itachezwa katika uwanja wa Bukhungu mjini Kakamega, Afraha Nakuru, Mumias Sports Complex na Moi, mjini Kisumu.

Hata hivyo, kuna wasiwasi michuano hii isifanyika MJINI Kisumu kwa hofu za kiusalama kwa mujibu wa chama cha soka nchini Kenya na sasa uwanja wa Machakos utatumiwa.