CAF-TP MAZEMBE

TP Mazembe yashinda tena taji la Shirikisho barani AFrika

TP Mazembe mabingwa wa taji la Shirikisho barani Afrika
TP Mazembe mabingwa wa taji la Shirikisho barani Afrika PHILL MAGAKOE / AFP

Klabu ya soka ya TP Mazembe kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilishinda taji la Shirikisho barani Afrika mwisho wa wiki iliyopita dhidi ya SuperSport United ya Afrika Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Fainali hiyo ya pili ilimalizika kwa timu zote mbili kutofungana, jijini Pretoria, lakini ushindi wa TP Mazembe wa mabao 2-1 juma moja lililopita wiki moja iliyopita mjini Lubumbashi.

Kocha wa TP Mazembe Pamphile Mihayo mwenye umri wa miaka 41, baada ya ushindi huu, amesema angependa kusalia katika klabu hiyo hata iwapo nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine.

Mihayo aliichezea TP Mazembe kama kiungo wa kati, na alionekuwa kuwa kiungo muhimu wakati wa michuano ya kombe la dunia kwa vlabu mwaka 2010, na kufika fainali dhidi ya Intermilan na kupoteza kwa mabao 3-0.

Kocha huyo ambaye amekuwa kocha tangu mwezi Aprili, amesema mafanikio hayo yamekuja kutokana na hatua ya wachezaji kumsikiliza na kumkubali kama kocha wao.

Mmiliki wa klabu hii Moise Katumbi Chapwe anayeishi nje ya nchi hiyo, amewasifia wachezaji wa klabu hiyo na kuwaelezea kama mashujaa waliopambana kutetea taji hili licha ya mazingira magumu.

Michuano hii ya Shirikisho ilianza mwaka 2004. Klabu ya kwanza kushinda ilikuwa ni Hearts of Oak ya Ghana.

CS Sfaxien ya Tunisia wanashikilia rekodi ya kushinda taji hili mara tatu mwaka 2007, 2008 na 2013.

Etoile du Sahel pia ya Tunisia nayo imeshinda taji hili mwara mbili mwaka 2006 na 2015.

FAR Rabat ya Morocco, Stade Malien ya Mali, FUS Rabat pia ya Morocco na MAS Fezm AC Leopards ya Congo na Al Ahly ya Misri wameshinda taji hili mara moja.

Bingwa wa taji hili huwa anacheza na bingwa katika michuano ya klabu bingwa kuwania taji la CAF Super CUP.

Mshindi wa mwaka huu, atajishindia Dola za Marekani Milioni 1.6.