Kenya waibuka mabingwa wa taji la CECAFA 2017

Sauti 23:24
Wachezaji wa Harambee Stars wakishangilia baada ya ushindi wa taji CECAFA
Wachezaji wa Harambee Stars wakishangilia baada ya ushindi wa taji CECAFA Goal.com

Kenya ndio mabingwa wa taji la soka la CECAFA, baina ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, baada ya kuishinda Zanzibar kwa mabao 4-3 kupitia mikwaju ya penalti. Hili ni taji lake la saba.