SOKA-TANZANIA

Droo ya

Wachezaji wa klabu ya Simba FC nchini Tanzania
Wachezaji wa klabu ya Simba FC nchini Tanzania allafrica.com

Droo ya hatua ya 32 bora ya kuwania taji la Shirikisho nchini Tanzania imetangazwa leo huku Yanga ikipangwa kukutana na Ihefu ya Mbeya. 

Matangazo ya kibiashara

Ihefu ilitinga hatua hiyo baada ya kuitoa Mbeya City kwa mikwaju ya penati.

Azam FC ambayo mwaka jana ilifika hatua ya nusu fainali na kufungwa na Simba kwa bao 1-0 itakutana na timu ya Shupavu FC.

Droo hiyo imefanyika asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na wadau mbalimbali wakiwemo wachezaji wa zamani wa klabu za Simba na Yanga, Yusuph Macho na Shekhan Rashid.

Mabingwa watetezi wa taji hilo Simba SC, waliondolewa katika hatua ya 32 na timu ya Green Worriors kwa mikwaju ya penati 4-3.

Ratiba ya michezo mingine ni kama ifuatavyo

 • KMV V Toto Africans 
 • Maji Maji v Ruvu Shooting
 • Njombe Mji v Rhino Rangers
 • Kiluvia Utd v JKT Oljoro
 • Ndanda Fc v Biashara United
 • Pamba SC v Stand United
 • Polisi TZ v Friends Rangers
 • JKT Tanzania v Polisi Dar
 • Mwadui FC v Dodoma FC 
 • Green Warriors v Singida United
 • Tanzania Prisons v Burkina Faso
 • Kariakoo United v Mbao FC
 • Maji Maji Rangers Lindi v Mtibwa Sugar
 • Kagera Sugar v Buseresere FC 

Michezo hiyo ya hatua ya 32 bora itachezwa Januari 31 na Februari 1.

Ripoti ya mwandishi wa RFI Kiswahili, Fredrick Nwaka