CAF-SOKA

Mohamed Salah mchezaji bora wa soka barani Afrika

Mohammed Salah, mchezaji bora barani Afrika
Mohammed Salah, mchezaji bora barani Afrika www.cafonline.com

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya soka ya Misri, anayecheza soka la kulipwa nchini Uingereza katika klabu ya Liverpool Mohamed Salah, ndiye mchezaji bora barani Afrika kwa mwaka wa 2017.

Matangazo ya kibiashara

Salah mwenye umri wa miaka 25, aliwashinda wenzake Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Gabon anayechezea klabu ya Borussia Dortmund pamoja na Sadio Mane kutoka Senegal lakini pia mchezaji wa Liverpool nchini Uingereza.

Mchezaji huyo wa Misri, alishinda taji hilo kutokana na mchango wake katika klabu ya Liverpool, ambako amefunga mabao 17 hadi sasa lakini pia aliisadia timu yake kufuzu katika michuano ya kombe la dunia itakayofanyika mwezi Juni mwaka huu nchini Urusi.

“Ningependa kutoa tuzo hii kwa watoto wote barani Afrika na nchini Misri,”.

“Nawaambia kuwa waendelee kuwa na matumaini na kufanya bidii kwa sababu wanaweza,” alisema Mohamed Salah.

Taji la mwanamke bora, lilimwendea Mnigeria Asisat Oshoala anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Dalian Quanjian nchini China.

Tuzo nyingine za CAF 2017:

Mchezaji chipikuzi wa mwaka : Patson Daka (Zambia na Liefering, Austria)

Kocha wa mwaka: Hector Cuper (Misri)

Timu ya taifa ya mwaka: Misri

Timu ya taifa ya wanawake ya mwaka: Afrika Kusini

Klabu bora: Wydad Casablanca (Morocco)

Kikosi bora cha mwaka 2017: Aymen Mathlouthi (Tunisia, Etoile Sahel); Ahmed Fathy (Misri, Al Ahly), Eric Bailly (Ivory Coast, Manchester Utd, Uingereza , Ali Maaloul (Tunisia, Al Ahly, Misri); Mohamed Ounnajem (Morocco, Wydad Casablanca).

Karim el Ahmadi (Morocco, Feyenoord, Uholanzi), Junior Ajayi (Nigeria, Al Ahly, Misri), Achraf Bencharki (Morocco, Wydad Casablanca); Khalid Boutaib (Morocco, Yeni Malatyaspor, Uturuki), Mohamed Salah (Misri, Liverpool, Uingereza), Taha Yassine Khenissi (Tunisia, Esperance)