UINGEREZA-SWANSEA-ARSENAL-MICHEZO

Swansea City yaiburuza Arsenal EPL

Koscha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger akisikitishwa na ushindi wa Swansea dhii ya klabu yake.
Koscha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger akisikitishwa na ushindi wa Swansea dhii ya klabu yake. Reuters/Carl Recine

Arsenal walilazwa na Swansea City katika michuano ya EPL kwa mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa siju ya Jumanne usiku. Kwa ushindi huo wa kwanza msimu huu, Swansea City imejizolea sifa kubwa na kuwapa masahabiki wake matumaini ya kuendelea kufanya vizuri.

Matangazo ya kibiashara

Katika dakika 33 ya kipindi cha kwanza Arsenal walikuja juu na kufunga bao la kwanza kupitia mchezaji wake Nacho Monreal. Hata hivyo Swanse walisawazisha dakika moja baadae kupitia mchezaji Clucas. Mechi hiyo ilipigwa katika uwanja wa Liberty Stadium.

Kosa la ajabu kutoka kwa Petr Cech lilimpa nafasi Jordan Ayew kufunga bao na kuwaweka Swansea kifua mbele kipindi cha pili kabla ya Sam Clucas kufunga bao lake la pilina hivyo Swansea kukamilisha mabao 3-1 hadi kipenga cha mwisho.

Swansea wameonekana kuimarika sana chini ya meneja mpya Carlos Carvalhal ambapo wameshindwa mechi moja pekee kati ya nane walizocheza.

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger aliwasifu wachezaji wa Swansea akisema kuwa “walikuwa makini sana, wenye nidhamu na hamu ya kutaka kushinda”.

Arsen Wenger amekosoa jinsi vijana wake walivyocheza.

“Nasikitika, na naamini kwamba hatukucheza kwa kiwango cha kutosha, naamini hatukuwa na nidhamu ya kutosha, “ alisema Wenger.