CAF-CHAN 2018

Morocco na Nigeria zafuzu fainali ya CHAN 2018

Morocco baada ya kufuzu katika fainali ya kuwania taji la CHAN Januari 31 2018
Morocco baada ya kufuzu katika fainali ya kuwania taji la CHAN Januari 31 2018 http://www.cafonline.com/

Morocco na Nigeria zitachuana katika fainali ya kuwania taji la CHAN kwa wachezaji wanaocheza soka katika ligi za nyumbani.

Matangazo ya kibiashara

Fainali hiyo itachezwa mjini Casablanca siku ya Jumapili, mchuano ambao utakuwa tamati ya michuano hii iliyoanza kutifua vumbi mwezi uliipita.

Wenyeji Morocco walikuwa wa kwanza kufuzu baada ya kuishinda Libya mabao 3-1 katika mchuano wa nusu fainali uliochezwa Jumatano usiku katika uwanja wa Mohammed wa Tano, mjini Casablanca.

Ayoub El Kaabi alikuwa wa kwanza kuifungia Morocco katika dakika ya 73 kipindi cha pili, lakini Abdulrahman Khalleefah aliisawazisha Libya katika dakika ya 86.

Mchuano huo ulilazimika kwenda katika muda wa ziada baada ya kukamilika kwa sare ya bao 1-1 lakini Ayoub El Kaabi alirejea tena katika dakika 97 na kufunga bao la pili

Mambo yalikuwa mabaya zaidi kwa Libya, baada ya Morocco kupata mkwaju wa penalti katika dakika 119, kupitia Walid El Karti.

Nigeria nao walipata ushindi wa bao 1-0, katika dakika ya 16 ya mchuano huo uliochezwa katika uwanja wa Marrakech.

Juhudi za Sudan kujaribu kusawazisha ziliambulia patupa, licha ya kujitahidi kushambulia ngome za Nigeria bila mafanikio.

Hii ndio mara ya kwanza kwa Morocco na Nigeria kufika katika hatua ya fainali ya michuano hii.

Mwaka 2014, Nigeria ilimaliza katika nafasi ya tatu.

Mbali na mchuano huo wa fainali, Libya na Sudan zitachuana katika mchuano wa kuwania nafasi ya tatu siku ya Jumamosi.