CHAN 2018-MOROCCO-NIGERIA-MICHEZO

CHAN 2018: Morocco yaiadhibu Nigeria 4-0

Wachezaji wa Morocco wakisherehekea ushindi wao na wafuasi wao.
Wachezaji wa Morocco wakisherehekea ushindi wao na wafuasi wao. FADEL SENNA / AFP

Morocco iliifunga Nigeria mabao 4-0 na kuibuka washindi katika michuano ya kombe la Afrika kwa wachezaji wa Ligi za ndani ( CHAN), mchezo uliopigwa jana Jumapili.

Matangazo ya kibiashara

Wenyeji Morocco walifanikiwa kulinyanyua taji la michuano hiyo kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Nigeria.

Bao la kwanza la Morocco lilipachikwa wavuni na Zakaria Hadraf muda mfupi baada ya kuanza kipinzi cha pili.

Dakika mbili baada ya kipindi cha mpumziko Peter Eneji Moses alitimuliwa uwanjani baada ya kupewa kadi ya pili ya njano kwa mchezo m'baya dhidi ya Mohammed Nahiri.

Bao la pili la Nigeria lilifungwa na Walid El Karti, huku Hadraf akipachika bao la tatu

Ayoub El Kaabi alikamilisha mchezo huo kwa kufunga bao la nne na hivyo kupelekea Morocco kutwaa taji la ichuano hiyo.

Mshambuliaji wa Morocco, Ayoub el-Kaabi aliyefunga bao la nne la Morocco dhidi ya Nigeria.
Mshambuliaji wa Morocco, Ayoub el-Kaabi aliyefunga bao la nne la Morocco dhidi ya Nigeria. Fadel SENNA / AFP