CAF-KLABU BINGWA AFRIKA-KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Yanga yaanza kwa ushindi mwembamba Ligi ya mabingwa Afrika

Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa ligi Kuu Tanzania Bara
Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa ligi Kuu Tanzania Bara rfi

Timu ya Yanga ya Tanzania imeanza michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika kwa kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya timu ya St.Louis ya Shelisheli.

Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo ni wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya mabingwa Afrika msimu wa mwaka 2018.

Bao pekee la Yanga katika mchezo huo limefungwa na kiungo wake Juma Mahadhi baada ya kutokea purukushani iliyotokana na kona iliyopigwa na Geofrey Mwashiuya.

Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, mahadhi alisema wapinzani wao walitumia mbinu ya kujilinda na hivyo kushindwa kutengeneza nafasi za nyingi za kufunga.

Kwa matokeo hayo,Yanga inahitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu hatua inayofuata ya michuano hiyo.

Matokjeo ya michezo mingine iliyokamilika

Cnaps ya Madagascar imeifunga Kampala City ya Uganda mabao 2-1

Gor Mahia imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Vegetarianos

JKU ya Zanzibar imetoka suluhu na Zesco ya Zambia

Zwsco ya Zambia imeichapa Armed Forces ya Gambia mabao 3-0

Katika michuano ya Kombe la Shirikisho matokeo ya michezo iliyochezwa hadi sa sasa ni kama ifuatavyo.

Ngazi Sports ya Comoro imetoshana nguvu na Port KLouis ya Mauritius kwa kufungana bao 1-1

Ripoti ya mwandishi wa RFI Kiswahili, Fredrick Nwaka