CAF-KLABU BINGWA AFRIKA-KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Simba yaanza kwa kishindo taji la Shirikisho Afrika

-
- CAF

Timu ya Simba ya Tanzania imeanza kwa kishindo michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika kwa kuishinda Gendermarie Nationale ya Djibout mabao 4-0.

Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo umechezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ambapo mabao ya Simba yamefungwa na Said Ndemla, Emanuel Okwi na mshambuliaji John Bocco aliyefunga mabao mawili katika mchezo huo.

Timu ya Gendermarie inayotoka nchini Djibout ilitumia muda mwingi wa mchezo kujilinda huku mara kadha wachezaji wake wakipoteza muda kwa kujiangusha.

Kwa matokeo Simba inahitaji sare ya aina yoyote katika mechi ya marudiano itakayochezwa wiki ijayo nchini Djibout ili kufuzu hatua inayofuata ya michuano hiyo ya pili kwa ngazi ya klabu barani Afrika.

Matokeo ya mechi nyingine za taji la Shirikisho zilizochezwa leo

AFC Leopards ya Kenya imefungana bao 1-1 na Foisar Junior ya Madagascar.

APR ya Rwanda imeishinda Anse Reunion ya Shelisheli kwa mabao 4-0

Ripoti ya mwandishi wa RFI Kiswahili, Fredrick Nwaka