KENYA-SOKA-AFCON 2019

Kocha wa timu ya taifa ya Harambee Stars Paul Put ajiuzulu

Kocha Paul Put
Kocha Paul Put www.completesportsnigeria.com

Kocha wa timu ya taifa ya soka nchini Kenya Paul Put ametangaza kujiuzulu.

Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Ubelgiji amesema ameacha kuifunza Harambee Stars kwa sababu za kibinafsi.

Shirikisho la soka nchini humo FKF, limesema hatua ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 61, ni pigo kwa jitihada za Harambee Stars kufuzu kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon.

Uongozi wa soka nchini humo umesema Stanley Okumbi ambaye alikuwa kocha msaidizi, kukaimu nafasi hiyo.

Kuondoka kwa kocha Put ambaye alipewa kazi kuifunza Kenya mwezi Novemba mwaka uliopita kwa muktaba wa miaka miwili, anaondoka wakati huu Harambee Stars ikijiandaa kucheza na Ghana katika mchuano muhimu wa kufuzu kucheza kombe la AFCON.

Kenya ilianza vibaya mwaka uliopita, baada ya kufungwa na Sierra Leone mabao 2-1.

Put aliwahi kuifunza Burkina Faso na Gambia.