FIA-KENYA-KUKIMBIZA MAGARI

FIA yataka Kenya kurejea katika mashindano ya dunia

Mashindano ya kukimbiza magari
Mashindano ya kukimbiza magari www.wrc.com/en/

Kiongozi wa Shirikisho la mchezo wa kukimbiza magari duniani FIA, ametoa wito kwa Kenya kuhakikisha kuwa usalama barabarani unarejeshwa ili nchi hiyo irejee katika mashindano ya Kimataifa ya dunia (WRC).

Matangazo ya kibiashara

Rais wa FIA Jean Todt amesema Kenya ina uwezo mkubwa katika mchezo huu na inastahili kurejea katika kalenda ya mashindano hayo.

Amefanya ziara nchini Kenya, kuthathmini usalama wa eneo la nchi hiyo kuwa na mashindano hayo makubwa duniani, miaka mitatu baada ya Kenya kutangaza kuwa ingependa kurejea katika mashindano hayo ya dunia.

Mwaka 2002, Kenya iliondolewa katika mashindano ya dunia kutokana na ukosefu wa usalama katika eneo la kukimbiza magari hayo lakini pia changamoto za kifedha.

Mkuu huyo wa FIA, ametaka barabara zinazotumiwa katika mashindano haya kutokuwa na makaazi makubwa ya watu ili kuepusha kuhatarisha maisha ya watu.

Serikali ya Kenya inasema imetenga Dola Milioni 2 kuisadia mashindano hayo kurejea katika medani ya kimataifa.