BEIJIN GUOAN-VILLARREAL-SOKA

Klabu ya Beijing Guoan yakamilisha mkataba wake na Cédric Bakambu

Cédric Bakamb, mchezaji wa kimataifa kutoka DRC wakati wa mazoezi ya klabu ya Beijing Guoan.
Cédric Bakamb, mchezaji wa kimataifa kutoka DRC wakati wa mazoezi ya klabu ya Beijing Guoan. HANDOUT / BEIJING GUOAN / AFP

Baada ya karibu miezi miwili ya kusubiri, klabu ya China ya Beijng Guoan itakamilisha rasmi leo Alhamisi asubuhi utaratibu wa kujiunga na klabu hiyo mshambuliaji wa klabu ya Villarreal Cédric Bakambu, baada ya kulipa Euro milioni 74.

Matangazo ya kibiashara

Utekelezaji wa mkataba huu wa kununuliwa kwa mchezaji wa DRC ulikua ukisubiriwa kwa karibu miezi miwili. Mapema mwezi Januari, Cédric Bakambu alifanyiwa uchungizi wa afya yake kabla ya kusaini kuichezea klabu ya Beijing Guoan misimu minne.

Awali klabu hiyo ililipa klabu ya Villarreal kitita cha Euro milioni 37. Lakini klabu hiyo ya China ilijaribu bila mafaniko kukwepa kodi mpya ya 100% iliyowekwa na serikali kwa ajili ya kujiunga na klabu za China kwa wachezaji wa kigeni.

Hata hivyo klabu ya Beijing Guoan ilitakiwa kulipa Euro milioni 74 kwa kumnunua mchezaji huyo wa DRC kutoka Vitry-sur-Seine aliyepata umaarufu huko Sochaux.

Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka DRC, mwenye umri wa miaka 26, ametambulishwa leo Asubuhi mbele ya klabu yake na atakua mchezaji ghali kutoka afrika katika historia ya soka barani humo na ambaye atalipwa mshahara wa Euro milioni 18 kila mwaka.