UEFA-REAL MDRID-PARIS SAINT-GERMAIN

Kocha wa PSG asema hakuna aibu ya kufungwa na Real Madrid

Unai Emery kocha wa klabu ya  PSG
Unai Emery kocha wa klabu ya PSG Captura de vídeo

Kocha wa klabu ya soka ya Ufaransa, Paris Saint-Germain Unai Emery amesema hakuna aibu ya timu yake kufungwa na Real Madrid ya Uhispania na kuondolewa katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Emery amesema kuondolewa katika hatua ya 16 bora, inasikitisha lakini kufungwa na Real Madrid sio aibu kwa sababu walistahili kufuzu katika hatua ya robo fainali.

Paris Saint-Germain ilifungwa na Real Madrid mabao 2-1 katika mchuano wa mzunguko wa pili baada ya kupoteza mchuano wa kwanza mabao 3-1.

Cristiano Ronaldo na Casemiro waliifungia Real Madrid mabao yaliyowapa ushindi katika mchuano uliochezwa ugenini.

Wawakilishi wa Ufaransa wameondoka katika michuano hii licha ya kuwa na rekodi ya kuwasajili wachezaji Neymar kutoka Barcelona na Kylian Mbappe kutoka Monaco kwa kiasi kikubwa cha fedha.

Liverpool nayo ilifuzu baada ya kuishinda Porto ya Ureno kwa jumla ya mabao 5-0. Mchuano wa kwanza timu hizo hazikufungana.

Ratiba ya michuano hii inaendelea siku ya Jumatano:-

Tottenham Hotspurs vs Juventus (2-2).

Mancheter City v Basel (4-0).

Michuano hii itaendelea wiki ijayo.