Pata taarifa kuu
CAF-SOKA

TP Mazembe yaanza kwa kishindo Ligi ya Mabingwa Afrika.

-
- CAF
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho barani Afrika, TP Mazembe imeanza kwa kishindo kampeni ya kuwania taji la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuizamisha UD Songo ya Msumbiji mabao 4-0.

Matangazo ya kibiashara

Mechi hiyo ya hatua ya kwanza imechezwa jana jijini Lubumbashi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika Uwanja wa Frederic Kibassa Maliba.

Mabao ya mazembe ambao ni mabingwa wa taji hilo mwaka 2015 yalifungwa na Malango Ngita aliyefunga mabao matatu na Muleka J aliyefunga bao moja.

Katika mchezo mwingine Difaa Al Jadida ya Morocco iliicharaza Vita Club ya DRC kwa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji kutoka Tanzania Simon Msuva.

Gor Mahia ya Kenya ilitoshana nguvu na Esperance ya Tunisia kwa sare ya bila kufungana wakati Zanaco ya Zambia ilishindwa kwa mabao 2-1 na timu ya mbabane Swallows ya Swaziland.

Wawakilishi wengine wa Afrika Mashariki, Rayon Sports ya Rwanda ilishindwa kutamba nyumbani kwa kutoka suluhu na mabingwa wa mwaka 2016, Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini.

Matokeo ya michezo mingine ya Ligi ya mabingwa Afrika yalikuwa kama ifuatavyo.

Zesco ilifungwa bao 1-0 na Asec Mimosas ya Ivory Coast

St. George ya Ethiopia ilitosha nguvu kwa sare ya bila kufungana na KCCA ya Uganda.

Wydad Casablanca iliishinda Williumsville ya Ivory Coast kwa mabao 7-2

Premeiro de Agosto ya Angola iliishinda Bidvest Wits ya Afrika Kusini kwa bao 1-0.

Adouana Stars ya Ghana iliishinda Entente Setif ya Algeria kwa bao 1-0

Mechi za marudiano zinatarajiwa kuchezwa katikati ya mwezi huu wa Machi.

Katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika matokeo ya mechi za jana

Simba ilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Al-Masry ya Misri

Olimpic Stars ya Burundi iliotoka sare ya bila kufungana na Hilal El Obeid ya Sudan

Waleyta Dicha ya Ethiopia ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Zamalek ya Misri

AS Maniema ya DRC ilifungana mabao 2-2 na USM Alger ya Algeria

Enyimba ya Nigeria iliishinda Energie Sports ya Benin mabao 2-0

APR ya Rwanda ilifungwa na Djoliba ya Mali kwa bao 1-0

Coast do Sol ya Msumbiji ilifungwa bao 1-0 na Cape Town City ya Afrika Kusini.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.