SOKA-UGIRIKI-SERIKALI

Serikali nchini Ugiriki yasimamisha ligi kuu ya soka

Mwenyekiti wa klabu ya PAOK Ivan Savvidis alivyovamia uwanja wa soka
Mwenyekiti wa klabu ya PAOK Ivan Savvidis alivyovamia uwanja wa soka www.dailymail.co.uk/sport

Ligi kuu ya soka nchini Ugiriki imesitishwa kwa muda usiojulikana baada ya Mwenyekiti  wa klabu ya PAOK kuvamia eneo la kuchezea akiwa na bastola.

Matangazo ya kibiashara

Naibu wa Michezo nchini humo Yiorgos Vassiliadis, amesema uamuzi huu umefikiwa baada ya kukutana na kufanya kikao cha dharura na Waziri Mkuu Alexis Tsipras kutokana na tukio hilo.

Serikali nchini Ugiriki inataka sera mpya ya soka kukubaliwa na wadau wote nchini humo kwa ushirikiano na Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, kabla ya kurejelewa kwa ligi hiyo.

Hati ya kukamatwa imetolewa kwa Mwenyekiti  wa klabu hiyo  ya PAOK, Ivan Savvidis mfanyibiashara na mwanasiasa mwenye asili ya Urusi ambaye aliingia eneo la kuchezea akiwa na bastola.

Savvidis alikwenda kumlalamikia  mwamuzi baada ya kukataa  bao lililokuwa limefungwa na klabu yake katika dakika ya 90 dhidi ya klabu ya AEK Athens.

Baada ya majibizano makali, mwamuzi huyo aliamua kukubali shinikizo na kuipa PAOK bao hilo.

Timu hizo mbili PAOK na AEK pamoja na Olympiakos Piraeus ziko mbioni kutafuta ubingwa soka nchini humo. .