UEFA-MANCHESTER UNITED-SEVILLA

Manchester United yalemewa na Sevilla michuano ya UEFA

Wissam Ben Yedde akisherehekea baada ya kuigunga Manchester United katika mchuano wa Sevvila Machi 13 2018 katika uwanja wa Old Trafford
Wissam Ben Yedde akisherehekea baada ya kuigunga Manchester United katika mchuano wa Sevvila Machi 13 2018 katika uwanja wa Old Trafford Reuters/Jason Cairnduff

Klabu ya Manchester United ya Uingereza,  imeondolewa katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya  UEFA baada ya kufungwa mabao 2-1 na klabu ya Sevilla ya Uhispania katika mchuano muhimu wa kufuzu katika hatua ya robo fainali.

Matangazo ya kibiashara

Wissam Ben Yedde aliifungia timu yake mabao yote mawili, katika mchuano ambao Manchester United walikuwa wenyeji Jumanne usiku  katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford.

Mchuano wa ugenini nchini Uhispania, timu hizo mbili hazikufungana.

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuondolewa kwa klabu yake sio kitu cha ajabu.

Aidha, amesema kuwa wachezaji wake hawakucheza vibaya licha ya kushindwa.

“Sifikirii mchezo ulikuwa mbaya,” alisema Mourihno.

“Sijutii chochote, nilikifanya kile kilichokuwa ndani ya uwezo wangu na wachezaji walifanya bidii sana.Tulijitahidi lakini tukafungwa.Huo ndio mchezo wa soka,” aliongeza.

Hii ni mara ya nne kwa Mourihno kupoteza katika hatua ya 16 bora ya michuano hii ya klabu bingwa barani Ulaya.

Sevilla inaungana na Liverpool, Manchester City, Juventus, Roma na Real Madrid katika hatua ya robo fainali.

Michuano ya ya kufuzu inamalizika siku ya Jumatano:

Chelsea vs Barcelona (1-1 matokea ya mchuano wa kwanza)

Bayern Munich vs Besiktas (5-0 matokea ya mchuano wa kwanza)